Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upinzani washinikiza Ma-DED wasitumike kwa chaguzi zijazo

59136 Waakurugenzipic

Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Vyama vinane vya upinzani nchini vimetoa tamko linaloshinikiza utekelezaji wa hukumu iliyoweka zuio la wakurugenzi wa miji, manispaa, majiji na wilaya kusimamia chaguzi licha ya Serikali kukata rufaa.

Wamesema rufaa iliyokatwa na Serikali haiwezi kusimamisha utekelezaji wa hukumu hiyo.

Vyama vilivyokutana leo Mei 22, 2019 jijini Dar es salaam ni ACT Wazalendo, CCK, NLD, NCCR Mageuzi, Chaumma, UPDP, Chadema na DP.

Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa Chaumma, ambaye pia kiongozi wa umoja wa vyama hivyo, Hashim Rungwe amepongeza uzalendo wa Bob Wangwe huku akilaani upotoshaji unaotokana na hukumu hiyo.

"Msimamo wa kisheria wa uamuzi wa Mahakama Kuu uko wazi, kwamba vifungu vya 7(1) na 7(2) ni batili, hii inamaanisha kuanzia siku ya hukumu ilipotolewa ni marufuku wakurugenzi kusimamia chaguzi, "amesema Rungwe aliyekuwa ameongozana na viongozi kadhaa wa upinzani.

Siku chache zilizopita Mahakama Kuu ilitoa hukumu iliyobatilisha kifungu cha 7(1) na 7(2) vya sheria ya uchaguzi vilivyokuwa vinaipatia NEC mamlaka ya kuteua wakurugenzi kusimamia chaguzi.

Habari zinazohusiana na hii

Hata hivyo Serikali imeshakata rufaa katika Mahakama ya Rufaa inayolenga utekelezaji wa hukumu hiyo katika chaguzi zijazo.

Akisoma maazimio ya vyama hivyo, Rungwe amesema wanajiandaa kufungua kesi nyingine mahakamani ili kushinikiza upatikanaji wa Tume Huru ya Uchaguzi, akisisitiza zuio la wakurugenzi pekee halitoshi.

Chanzo: mwananchi.co.tz