Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upinzani wanusa upigaji marekebisho viwanja vya michezo

Uwanja Wa CCM Kirumba 1140x640 Upinzani wanusa upigaji marekebisho viwanja vya michezo

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vyama vya upinzani nchini vimekosoa mpango wa serikali wa kutumia mamilioni ya dola za walipa kodi kukarabati viwanja kadhaa vikiwemo vinavyomilikiwa na chama tawala CCM.

Wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara yake, Waziri wa Utamaduni na Michezo aliliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha shilingi bilioni kumi ambazo ni sawa na dola za Marekani milioni 4.2 zitakazotumika kukarabati viwanja saba vya michezo, vitano vikiwa vya CCM.

Pendekezo hilo limeibua maswali makali kutoka kwa wanachama wa upinzani ambao wameutaja mpango huo kuwa ni ubadhirifu wa fedha za umma.

Naibu msemaji huyo wa masuala ya michezo na utamaduni kutoka chama cha upinzani cha ACT Wazalendo, alisema serikali inapaswa kurejesha umiliki wa viwanja hivyo kwa serikali kabla ya kuvifanyia ukarabati.

John Mrema, kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliliomba Bunge kukataa pendekezo hilo akisema ni jambo lisilokubalika kutumia fedha za walipa kodi kukarabati majengo ya watu binafsi.

Wizara hiyo imetetea pendekezo lake ikisema huduma hizo hazitatumiwa na wana CCM pekee, bali Watanzania kwa ujumla.

Tanzania inajitahidi kuboresha vifaa vyake vya michezo kama mkakati wa kuwezesha taifa la Afrika Mashariki kufuzu kuandaa michuano mikubwa ikiwemo Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live