Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upinzani wahoji unyanyasaji unaofanywa na TRA

57420 Trapic

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeitaka Serikali ya Tanzania kutoa kauli kuhusu vitendo vinavyofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) vya kuwapangia bei ya bidhaa wafanyabiashara wa mkoa wa Dar es Salaam.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Mei 14, 2019 na msemaji wa kambi hiyo wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Cecil Mwambe.

Mwambe amesema TRA mkoa wa Dar es Salaam wameanzisha utaratibu wa kuvizia wateja wanaotoka madukani kununua bidhaa huku wakiwa na risiti mikononi mwao.

“Mara wanapomuona mtu ametoka dukani, humuamuru kuonyesha bidhaa alizonunua na sehemu aliponunulia. Yapo malalamiko ya kwamba mara wanapoonyeshwa duka husika maofisa hao wa TRA hupanga bei zao dukani na kudai bidhaa iliyouzwa na kutolewa risiti imeuzwa kwa kiwango cha chini,” amesema.

Amesema maofisa hao humtaka mwenye duka kufika TRA na au kuwasiliana na maofisa hao na kwamba hali hiyo ipo kwenye maduka ya Kariakoo kuelekea Jangwani ambako wananchi hununua bidhaa za kwenda mikoani.

 

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz