Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upigaji kura wachelewa kuanza Kata ya Nsalaga-Mbeya

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Shughuli ya kupiga kura kwenye baadhi ya vituo vya kata ya Nsalaga jijini Mbeya imechelewa kwa dakika 40.

MCL digital imefika kwenye vituo sita vilivyopangwa kwa ajili ya kupigia kura leo Septemba 16 na kukuta foleni ya wananchi wakisubiri shughuli hiyo kuanza.

Vituo vilitakiwa kufunguliwa saa Moja asubuhi, lakini ilishindikana licha wapiga kura kujitokeza kabla ya muda huo na saa 1.40 asubuhi ndipo shughuli ya wakazi wa Nsalanga walianza kupiga kura zao.

Mmoja wa wananchi waliofika katika kituo cha shule ya msingi Nsalaga, Antony Simon amesema ameshangazwa na kitendo hicho cha kuchelewesha kuanza kupiga kura wakati walitangaziwa kazi ya kupiga kura ingeanza saa moja kamili asubuhi.

"Watu tumewahi hapa tangu Saa 10:00 alfajiri, lakini cha ajabu mpaka sasa hakuna kinachoendelea na maelezo wanayotupatia hawa wasimamizi wa kituo hayaeleweki na ukizingatia watu tumeacha shughuli zetu ili tuwahi kuwachagua viongozi wetu tukaendelee na majukumu mengine,” amesema Simon.

Naye Nuru Ntature mkazi wa Nsalaga amesema kilichotokea kwenye baadhi ya vituo ni kutokana na wasimamizi wa uchaguzi kutokujiandaa mapema hali iliyosababisha usumbufu kwa wananchi waliojitokeza kwa kuambiwa wino bado haujafika.

Msimamizi wa uchaguzi kituo cha Nsalaga, Antony Kasebwa amesema kazi hiyo  imechelewa kutokana na makubaliano maalumu ya mawakala wa vyama vyote kwa sababu kuna mambo wanataka kujiridhisha kabla ya kazi kuanza.

Chanzo: mwananchi.co.tz