Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upatikanaji wa maji mjini sasa ni 86%- CCM

Kero Majipic CCM yatamba kuboresha huduma ya maji mijini

Thu, 9 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amesema kwamba baada ya miaka 60 ya Uhuru, upatikanaji wa maji katika miji umeongezeka hadi kufikia asilimia 86

Kauli hiyo ameitoa hii jana Desemba 8, 2021, Dar es Salaam, wakati akizungumzia mafanikio yaliyopo baada ya miaka 60 ya Uhuru, wapi walikotoka na wapi ilipo serikali inayoongozwa na chama hicho, huku akiahidi kwamba chama hicho kitaendelea kujenga Tanzania imara katika nyanja mbalimbali za amendeleo.

"Nchi yetu wakati inapata Uhuru, upatikanaji wa maji katika miji yetu ulikuwa kwa asilimia 25 tu kuna miji ilikuwa inapata maji kwa asilimia 8, 6 ama 10, lakini leo miaka 60 baada ya Uhuru upatikanaji wa maji ni asilimia 86, tuko kwenye kiwango kizuri," amesema Chongolo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live