Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uongozi wa kuwagawa watu unaturudisha nyuma – CCM

Nchimbi Ccm (22).jpeg Uongozi wa kuwagawa watu unaturudisha nyuma – CCM

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema chama hicho hakitaki uongozi wa kuwagawanya watu kwakuwa unapeleka mpasuko na kukwamisha maendeleo.

Nchimbi ameyasema hayo hii leo Aprili 13, 2024 katika ziara yake Mkoani Katavi na kuongeza kuwa moja ya changamoto kubwa iliyopo ndani ya CCM ni tabia ya baadhi ya viongozi wanaoshindwa na wanaoshinda kutokukubali matokeo mioyoni mwao.

Amesema, “Chama cha Mapinduzi hakitaki na kinakemea tabia ya Uongozi wa kugwanya watu kwakuwa unapelekea mpasuko ndani ya Chama na kukwamisha maendeleo kwa Watanzana.”

Amebainisha kuwa, “moja ya changamoto kubwa iliyopo ndani ya CCM ni tabia ya baadhi ya viongozi wanaoshindwa na wanaoshinda kutokukubali matokeo miyoyoni mwaona matokeo yake pamoja na uchache wao lakini wanakuwa na madhara makubwa na kusema tabia hiyo iachwe mara moja kwakuwa ni ujinga na sio misingi ya demokrasia.”

“Unakuta mtu kagombea na kashinda lakini akimaliza kushinda anaanza kutafuta nani hakumuunga mkono ili apambane nae na kumkandamiza, hiyo ni tabia ya kijinga na haiungwi mkono, tuache mara moja,” alisema Balozi Dkt. Nchimbi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live