Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unguja ni haluwa, kahawa kupongezana

47721 Pic+halua

Wed, 20 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Kila kukicha ni afadhali ya jana kutokana na harakati za kukua na kuenea kwa chama cha ACT- Wazalendo kushika kasi visiwani Zanzibar.

Baada ya jana Jumanne Machi 19,2019 kuonekana matawi mengi yakipandishwa bendera za ACT-Wazalendo ambacho aliyekuwa katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuamua kujiunga nacho baadhi ya wafuasi wake wameonekana kufanya sherehe mbalimbali visiwani hapa.

Furaha hiyo ambayo Mwananchi Digital imeishuhudia leo Jumatano Machi 20,2019 katika baadhi ya viunga vya mji Mkongwe Mjini Unguja, kumekuwa na shughuli maalumu ya ugawaji halua na kahawa kama ishara ya wananchi hao kufurahia na baadhi ya maeneo yakionekana kuwapo shughuli za uchinjaji wa mbuzi.

Kawaida matokeo haya visiwani hapa huashiria uwapo wa furaha ya jambo ambalo watu huamua kupongezana kama ishara ya ushindi, au sherehe maalumu zikiwamo za harusi au maulidi.

Mwananchi Digital ilibahatika kuzungumza na aliyekuwa katibu wa CUF Jimbo la Malindi Ahmed Bashuti, amesema shughuli hiyo itakuwa endelevu katika matawi ya jimbo hilo.

Amesema wameona ni vyema kufanya tafrija baada ya kuona wananchi  wengi hivi sasa wamekuwa huru na kutoka kwenye kifungo walichokuwamo CUF.

Mmoja wa wafuasi waliohudhuria sherehe hiyo Said Shaib, amesema wamepata faraja kubwa ndani ya nyoyo zao hasa kwa kiongozi wao ambaye ni Maalim Seif kutangaza rasmi kujiunga na ACT-Wazalendo



Chanzo: mwananchi.co.tz