Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unajiita Mheshimiwa huna mshahara? - Kinana

Kazi Ya Serikali Ni Kutengeneza Miundombinu   Kinana.jpeg Abdulrahman Kinana.

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesema kinachowaponza madiwani na wabunge ni kujiita waheshimiwa.

Kinana ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara mkoani Tabora ambapo alishangazwa na madiwani kujiita waheshimiwa wakati hata mishahara hawana.

“Madiwani wanalipwa posho tu hawana mishahara kwa sababu wanaojiita waheshimiwa basi mtu ana shida yake binafsi anaenda kwa diwani ampe hela, anauguliwa diwani ndio atoe pesa ya matibabu, anasafari zake binafsi diwani ndio atoe pesa, akisema hana nongwa, tutakukata 2025.

“Wabunge wetu ndio wanaolipwa mshahara mdogo kuliko wabunge wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Congo, Kenya, Uganda, Rwanda ukicheki mishahara ya wabunge Iko juu kuliko wabunge wetu wa Tanzania na tukisema tuwaongeze mtasikia kelele zake.

“Wabunge wakirudi jimboni kila mtu hodi anataka apewe hela, wakati mwingine mtu anafunga safari nauliza hana mbunge ndio ampe, akasema hana nongwa, 2025 tunakutoa, si sawa hata kidogo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live