Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umri wa mgombea wageuzwa ajenda

10295 Pic+umri TanzaniaWeb

Mon, 6 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Missenye. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetetea umri wa mgombea wake, Francis Mutasa (pichani) katika Kata ya Minziro baada ya upande wa upinzani kuamua kugeuza kuwa ‘hoja kuu’ kwenye mikutano yao ya kampeni.

Akihutubia mkutano wa kampeni katika kata hiyo, katibu wa itikadi na uenezi wa Mkoa, Hamimu Mohamud aliwataka wananchi kupuuza madai ya mgombea wao kuwa na umri mkubwa kwani pamoja na umri huo bado anao uwezo wa kutekeleza ilani ya chama.

“Ni kweli umri wake umekwenda akilinganishwa na mgombea mwenzake ana umri kati ya 68 na 72 tunataka mtu anayejua historia,” alisema Mohamud alipokuwa akitetea umri wa Mutasa.

Alisema mgombea wao alikuwa miongoni mwa vijana wa CCM waliokwenda nchini Uganda wakati wa vita ya kumng’oa dikteta Idd Amin na kuwa umri wake isiwe kigezo cha kutaka asifaidi matunda ya Uhuru aliyopigania.

Mohamud aliwaeleza wananchi kuwa mgombea wao atalinda historia ya kata hiyo iliyopo mpakani na nchi jirani na Uganda na kuwa anajua kero zinazowakabili wananchi kwa kuwa alikuwa katibu kata wa eneo hilo.

Katika mkutano huo, mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Costancia Buhiye alisema mgombea aliyefariki alitokana na chama hicho na wamemleta mgombea atakayeendeleza mipango iliyoachwa na mtangulizi wake.

Aliwaomba wananchi kumchagua mgombea wao chama hicho kwa kuwa ana uwezo wa kutekeleza ilani ya chama hicho kwa kushirikiana na viongozi wengine ndani ya chama.

Chanzo: mwananchi.co.tz