Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umoja wavitesa vyama vya upinzani

Ukawa+pic Umoja wavitesa vyama vya upinzani

Fri, 5 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SIKU chache baada ya vyama vya Chadema na NCCR–Mageuzi, kutangaza kufungua milango kwa vyama vingine vya upinzani vilivyotayari kushirikiana kuikabili CCM , ACT-Wazalendo imefunguka.

Juzi Chadema ilitangaza kufungua milango kwa vyama vya upinzani kushirikiana navyo kuing’oa CCM, na jana NCCR –Mageuzi ilitangaza jambo hilo hilo.

Kutokana na hali hiyo, Nipashe iliviuliza vyama ambavyo havijazungumzia ushirikiano huo, na ACT-Wazalendo kilisema nia na dhamira yake ya siku nyingi ya kushirikiana na vyama vingine kueleka Oktoba iko pale pale.

Naibu Katibu wa Uendezi Habari na Mahusiano kwa Umma wa chama hicho, Janeth Rithe, akizungumza na Nipashe alisema kwa muda mrefu chama hicho kilizungumzia ushirikiano huo na wapo tayari kushirikiana na chama chochote.

“Mdau mkubwa wa kwanza ambaye anataka ushirikiano na vyama vingine vya siasa vya upinzani ni ACT-Wazalendo, tulishaanzisha mazungumzo na vyama mbalimbali, ili tushirikiane kwenye uchaguzi na kwenye kutoa misimamo ya vyama,” alisema.

Alisema hivi sasa bila ya kuwa na umoja na kuzungumza na kutoka na kauli moja kunakuwa na mgawanyiko.

CUF: TUNASUBIRI VIKAO

Naye, Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya, alisema mambo yao mengi huamuliwa kwenye vikao ambavyo vinatarajia kuanza mwishoni mwa wiki ijayo.

“Maandalizi yetu ya uchaguzi na mambo mengine yanayojitokeza kama kuna umuhimu au hakuna umuhimu yatategemea na vikao vya maamuzi ambavyo vitaanza mwishoni mwa wiki ijayo, tutashauriana kuona kama kuna ulazima au hakuna ulazima,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live