Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulinzi waimarishwa uchaguzi CCM Mara

Ulinzi Ulinzi waimarishwa uchaguzi CCM Mara

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mara kikitarajiwa kufanya uchaguzi wake leo Jumatatu, Novemba 21, 2022 kwa ajili ya kupata viongozi wake, ulinzi umeimarishwa kwenye ofisi za chama hicho na maeneo yaliyo jirani.

Ulinzi huo unahusisha kufungwa kwa barabara za kuingia na kupitia jirani na ofisi hizo huku kukiwa na ulinzi wa askari polisi pamoja na mgambo kwenye barabara hizo zilizofungwa.

Barabara za kupita na kuingia katika ofisi za CCM zimefungwa takriban mita 150 kutoka geti kuu la ofisi za CCM kwa pande tatu ambapo kila gari linalopita katika barabara hizo lazima kusimama na kujitambulisha kabla ya kuruhusiwa kuendelea na safari.

Katibu wa CCM mkoa wa Mara, Lengael Akyoo amesema wameamua kufunga barabara hizo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na barabara hizo kupitisha watu wengi kuelekea maeneo tofauti ikiwepo kwenye ofisi za CCM mkoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live