Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukata wakwamisha wagombea wa TLP Tandahimba

85738 Pic+tlp Ukata wakwamisha wagombea wa TLP Tandahimba

Mon, 25 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tandahimba. Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) katika wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara nchini Tanzania kimelazimika kumsimamisha mgombea mmoja pekee katika nafasi ya kitongoji kati ya vitongoji 650 vilivyopo baada ya wagombea wake kutakiwa kujigharamia.

Katika wilaya hiyo chama pekee cha upinzani kilichosimamisha wagombea ni TLP katika nafasi moja ya mwenyekiti wa kitongoji cha Kiwanjani kata ya Tandahimba akichuana na mgombea wa CCM na wagombea wengine wawili wakishiriki uchaguzi wa nafasi mchanganyiko katika kijiji cha Nahnyanga C huku CCM ikiwa na wagombea kumi.

Akizungumza baada ya kupiga kura leo Jumapili Novemba 24, 2019, katibu wa TLP wilayani humo, Ally Chitowa ambaye pia ni mgombea pekee wa kitongoji hicho anayewania nafasi hiyo kwa mara ya tatu amesema kutokana na uwezo mdogo wa chama wagombea walitakiwa kujigharamia na hivyo kugombea nafasi hiyo moja.

Amesema chama hicho kimetendewa haki katika uchaguzi huo na ndio sababu wameshiriki uchaguzi.

“Tulitarajia maeneo yote tushiriki lakini ilifikia hatua ya kujitegemea lakini  wenzangu wote wakawa wameshindwa na hawakutoa taarifa yoyote ya kushiriki tena kwa sababu ya kukosa gharama, unakosa bendera, unakosa fulana, huwezi kuingia kwenye uchaguzi bila hata kiashiria,” amesema Chotowa

Pamoja na changamoto zilizopo katibu huyo amesema wanatarajia ushindi na kutokana na ukubwa wa kitongoji hicho kinatosha kupeperusha bendera yao katika wilaya hiyo.

“Kama katibu nimepokea kwa masikitiko sana kukosa viti kutokana na hali ilivyo ngumu, nilikuwa naomba chama kijipange uchaguzi ujao kisirudie makosa kama haya tusimame kama wanavyosimama vyama vingine isifikie wagombea kujitegemea wenyewe ilihali mazingira yamemzunguka vibaya,” amesema Chitowa

Chanzo: mwananchi.co.tz