Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Udini na Ukabila vyatajwa kampeni za kuwania Unaibu Spika

Lusinde Mbunge wa Mtera, Livingston Lusinde

Mon, 7 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde maarufu Kibajaji amesema kuna kampeni chafu kuelekea uchaguzi wa Naibu Spika wa Bunge, akidai kuwa zinalenga kuwagawa wabunge.

Kibajaji ametoa kauli hiyo nje ya viwanja vya Bunge leo Jumatatu Februari 7, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa kampeni za wagombea wa nafasi ya Naibu Spika.

Jumla ya wabunge 11 wa CCM wamejitokeza kuomba kuteuliwa kukiwakilisha chama hicho kugombea nafasi ya unaibu Spika kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Tulia Akson ambaye alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge hilo.

View this post on Instagram

A post shared by Mwananchi (@mwananchi_official)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live