Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchaguzi jimbo la Liwale kufanyika Oktoba 13

13808 Uchaguzi+pic TanzaniaWeb

Sat, 25 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Liwale Mkoa wa Lindi, utafanyika Oktoba 13 baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Zuberi Kuchauka (CUF) kujiuzulu na kujiunga na CCM.

Akitangaza uchaguzi huo Jijini Dar es Salaam leo Agosti 25, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage amesema tangazo la uchaguzi linakuja baada ya Tume kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Tanzania.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge, ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, ameitaarifu Tume kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Liwale Mkoa wa Lindi, kuanzia tarehe 13 Agosti, 2018,” amesema Jaji Kaijage

Akizungumzia  ratiba ya uchaguzi huo mdogo, Jaji Kaijage amesema, fomu za uteuzi zitatolewa Septemba 7 hadi 13  mwaka huu na uteuzi wa wagombea utafanyika Septemba 13 mwaka huu.

Taarifa hiyo imesema kampeni za uchaguzi zitaanza Septemba 14 na kumalizika Oktoba 12 mwaka huu na siku ya uchaguzi itakuwa  ni Oktoba 13 mwaka huu.

“Tume inavikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, miongozo, na maelekezo yote wakati wa kipindi cha uchaguzi huo mdogo,” Jaji Kaijage amesema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz