Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchaguzi Serikali za mitaa kufanyika tofauti Wilaya ya Mbozi

69049 Pic+mbozi

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbozi. Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeagizwa kutafuta maeneo ambayo si makazi ya watu na yasiyo na ofisi za vyama vya siasa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Julai 31, 2019 na katibu tawala msaidizi anayeshughulikia serikali za mitaa,  Lauteri Kanoni katika kikao cha baraza la madiwani  halmashauri ya Mbozi.

Amesema halmashauri hiyo ina maeneo 407 yasiyo na sifa za kufanyika uchaguzi kutokana na kuwa na nyumba za watu binafsi na vyama vya siasa.

"Maeneo mengi yapo kwenye nyumba za watu, ofisi za vyama vya siasa kwa vyovyote maeneo haya sio huru kwa uchaguzi,” amesema Kanoni.

Ameziagiza kamati za maendeleo za kata kuanza kutafuta maeneo mapya na huru yatakayotumika kufanyia uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba, 2019.

Kanoni amefafanua kuwa wilaya ya Mbozi inatarajiwa kuwa na maeneo 700 yatakayotumika kwa uchaguzi na kati ya maeneo hayo, yanayofaa kutumika ni 293.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz