Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uamuzi mpya wa UVCCM baada ya Lowassa kurejea.

46065 Pic+uvccm Uamuzi mpya wa UVCCM baada ya Lowassa kurejea.

Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amesema wamesahau na kumsamehe Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa baada ya kukiri makosa na kujirekebisha.

James amesema hayo leo Jumatatu Machi 11, 2019 jijini Dodoma wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuwa kama akitokea mtu akahoji kwa nini Lowassa amesamehewa na kukubaliwa na CCM anyooshe mkono kwamba yeye hana dhambi.

"Amekiri na anaanza upya na ndio maana hakurudishiwa uanachama wake wa zamani bali ameenda katika tawi lake na kuomba upya uanachama wa CCM.”

“Kila anayetaka kuwa mwanachama anatakiwa kufuata utaratibu kama wanachama wengine wanavyofanya," amesema.

Amehoji waliobainika kuhusika katika ripoti ya ukaguzi wa mali za CCM kama yupo aliyepelekwa mahakamani kwa makosa na kwamba anayekiri makosa yake na kujirekebisha husamehewa.

Lowassa ambaye alikuwa mwana CCM kabla ya Julai 28, 2015 kutangaza kujiunga na Chadema kisha Mei Mosi, 2019 mwanasiasa huyo alitangaza kurejea chama chake cha zamani cha CCM.

Related Content

Jumamosi iliyopita ya Machi 9, 2019 Lowassa alikwenda katika tawi la CCM, Monduli mkoani Arusha ambako alikabidhiwa kadi ya CCM kisha akazungumza na umati wa wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.

“Nimerudi nyumbani msiniulize nimerudi kufanya nini, nimerudi nyumbani,” alisema  Lowassa siku hiyo baada ya kukabidhiwa kadi.

Soma zaidi: Lowassa kutikisa uchaguzi CCM



Chanzo: mwananchi.co.tz