Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UWT waupongeza uongozi wa Wilaya ya Nachingwea

UWT Waupongeza Uongozi Wa Wilaya Ya Nachingwea.png UWT waupongeza uongozi wa Wilaya ya Nachingwea

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) wameupongeza uongozi wa wilaya ya Nachingwea Kwa kutekeleza miradi vizuri kama ambavyo ilani ya CCM inavyotaka. Akizungumza wakati akikagua miradi ya maendeleo mwenyekiti wa UWT taifa Merry Chatanda alisema kuwa amekagua miradi ya maji, ujenzi wa magengo mapya katika hospital ya Nachingwea pamoja,ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya Nachingwea na mradi wa kimaendeleo wa UWT Nachingwea wameiona inaendana na thamani ya fedha iliyotumika.

Chatanda alisema kuwa serikali ya wilaya ya Nachingwea inayoongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mohamed Hassan Moyo imekuwa makini kwa kufanya kazi Kwa umakini mkubwa.

Alisema kuwa chama cha mapinduzi wilaya ya Nachingwea inafanya kazi vizuri na kwa ushirikiano mkubwa na serikali ya wilaya hiyo na kuleta maendeleo ya wananchi kama ambavyo ilivyojionea.

Mwenyekiti wa UWT taifa Merry Chatanda alisema kuwa RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia suluhu Hassan anafanya kazi kubwa hivyo wananchi na Wanachama wa CCM wanatakiwa kumsemea mema anayoyafanya Kwa watu ambao wanambeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live