Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UWT waagizwa kuacha mifarakano chaguzi za ndani

Wanawakeeee Wanawake waagizwa kuacha mifarakano baada ya uchaguzi wa ndani

Mon, 20 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi zoezi la uchaguzi mkuu ndani ya Chama cha Mpainduzi (CCM ) ukiendelea kwa ngazi mbalimbali za jumuiya na Chama nchini,Jumuiya ya moja wa wanawake (UWT) imewataka wanawake kuacha mitafaruku na mifarakano baada ya uchaguzi huo.

Agizo hilo limetolewa na mwenyekiti wa UWT Taifa na mjumbe wa kamati kuu Bi.Gaudentia Kabaka wakati akizungumza na wanawake mkoani Njombe alipofanya ziara ya kikazi na kwamba kumekuwapo na viashiria vya mifarakano baina yao ndani ya Chama.

“Tusiwe tumesambaratishana,tumenuniana,tumekosana na tumeachana njioa kuelekea 2025.Kwasababu UWT ni jeshi kubwa hatuwezi kusambaratishana halafu tukaja kushinda”alisema Kabaka

Awali mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Scolastika Kevela amesema UWT Mkoa wa Njombe ipo imara katika kuhakikisha jumuiya hiyo na Chama kwa ujumla kinasonga mbele.

“Jumuiya yeti kuna utulhvu na ukiona utulivu huy ujue kuna mwenyewe niwahakikishie kuwa jumuiya yetu tunapendana na kushirikiana huku tukiongozwa na jemedari wetu mkuu mama Samia suluhu Hassan

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe Ndugu Abdulah Hassan Mwinyi anasema kwa sasa Chama kimesimamisha zoezi la kuwasajili wanachama wapya hadi uchaguzi wa ndani ya Chama utakapokwisha huku Akishindwa kujizuia kueleza mazuri anayoyafanya Rais Samia Suluhu Hassan.

Katibu tawala mkoa wa Njombe Bi.Judica Omary anasema serikali na Chama tawala vina mashirikiano makubwa na ya karibu katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi mkuu huku mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa akikiri kuwapo kwa hatua kubwa za maendeleo yanayopigwa mkoani hapo pamoja na kutekeleza kwa kiwango kikubwa maelekezo ya serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live