Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UVCCM na tambo mikutano ya hadhara

CCM WEB UVCCM na tambo mikutano ya hadhara

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Umoja wa Vijana UVCCM mkoa wa Songwe Fatuma Hussein amesema wanaanza kusafisha njia kabla ya kuanza mikutano ya hadhara katika mji wa Tunduma kwa kutembelea wafanya biashara na wajasiriamali.

Amesema katika ziara hiyo watajikita kuangalia changamoto mbalimbali za wajasiriamali na wafanyabiashara wa mji wa Tunduma ambao upo mpakani na Nchi ya Zambia na kuwaeleza mazuri ambayo yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

"Tunajaribu kutest mitambo kabla ya kuanza mikutano ya hadhara ambayo imeruhusiwa hivi karibuni na Rais Samia, Leo Hapa Tunduma tutatembelea soko la machinga lililopo Iboya, Soko la Majengo, ofisi za Bajaj zilizopo Majengo,

Sehemu nyingine ni kijiwe cha Bajaj , Ofisi za Bodaboda, shule ya Sekondari Maporomoko na kuongea na Wananchi katika eneo la kubadilishana fedha Kisimani," amesema Fatuma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live