Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UVCCM Taifa kupata viongozi wapya leo

Uvccm Tiafa.jpeg UVCCM Taifa kupata viongozi wapya leo

Sun, 27 Nov 2022 Chanzo: Mwananchi

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wanatarajia kupata viongozi wapya leo Jumapili Novemba 27, 2022.

Viongozi hao watapatikana katika mkutano Mkuu wa 10 wa umoja huo ambao utaenda pamoja na Uchaguzi. Viongozi watakaochaguliwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watatu wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Tanzania Bara na wawili Tanzania Visiwani, wajumbe watatu wa Baraza Kuu UVCCM Tanzania Bara na wawili Tanzania Zanzibar.

Pia watachagua wajumbe wa UVCCM wanaowakilisha Wazazi na UWT.

Juni 2021 Rais Samia Suluhu Hassan alimteua aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja huyo, Kheri James kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo hivyo nafasi hiyo kubaki wazi.

Wagombea wanne wamepitishwa kugombea nafasi hiyo ambao wote wanatoka Zanzibar, wagombea hao ni Farid Mohammed Haji, Kassim Haji Kassu, Mohammed Ali Mohammed (Kawaida) na Mohammed Ibrahim Natepe.

Kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti wagombea ni Khadija Ismail, Dorice Mgeta, Victoria Mwanziva na Rehema Omary.

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Viti vitatu Tanzania Bara, wagombea ni Lulu Mwacha, Joachim Abel, Selestine Ojode, Isnail King, James Mwakibinga, Musa Mwakitinya, Janeth Mnyaga.

Wagombea wengine ni Janeth Kinawilo, Japhari Mghamba, Jackline Mnyanya, Edina Kakwene, Ramadhan Mlao, Queenelizabeth Makune na Khalid Mwinyigogo.

Kwenye nafasi ya Halmashauri Kuu CCM Taifa (NEC) Zanzibar viti viwili wagombea ni Atrash Abrahaman, Asha Ali Hassan, Mohammed Haji, Mwanaenzi Hassan Suluhu,Muhsin Haji Ussi,Omari Justas Moris na Stela Mbalawa.

Chanzo: Mwananchi