Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UVCCM Dar kuja kidigitali, wazindua mfumo mpya ‘Kazi Data’ (Video)

Video Archive
Mon, 12 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

UMOJA WA VIJANA CCM (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, imeandaa mfumo wa mpya wa Kazidata (Databases) utakaosaidia kuwatambua vijana wa ummoja huo na kupata taarifa zao.



Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi kompyuta mapakato(Laptop) 20 zitakazo saidia kuanzishwa kwa mfumo huo Akizungumza leo hii jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Baraza Kuu taifa UVCCM wa Mkoa wa Dar es salaam Gwantwa Alex Mwakijungu , amesema kuwa kuanza kwa mfumo huo utasaidia Sana Jumuiya ya vijana wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, kutunza kumbukumbu zake.

“Mimi nime amua kutoa hizi kompyuta ili ziweze kusaidia kuanza kwa mfumo huu kama alivyoshauri Mwekiti CCM Taifa Dr John Pombe Joseph Magufuli kuwa vijana tuwe wabunifu na kusaidia chama naamka ni hiki nilichukua kitoa kitasaidia kwa kiasi fulani” Alisema Gwantwa” Alisema Mwakijungu.

Naye Katibu wa uhamasishaji na chipukizi mkoa wa Dar es Salaam, Saady khimji amemshukuru Mjumbe huyo kwa msaada huo na kusema kuwa msaada huo umekuja wakati mwafaka unapokuwa anzishwa mfumo mpya na ametoa tahadhali kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam kutoshiriki maandamano haramu yanayo andaliwa katika mitandao ya kijamii.

Adelard Kiliba kutoka kampuni GPITG (LTD ) ambaye ni mtaalamu wa mfumo huo amesema Mfumo huo utajulikana kama UVCCM DATABASE SYSTEAM (DAUDAS) utasaidia pia kuweka kumbukumbu ya nguvu kazi na lasilimali watu,na utakuwa na mfumo wa kihasibu na Wanachama watafanya malipo ya Ada yatafanyika humo humo na unatarajiwa kuanza kutumika April mwaka huu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Ilala Hamad Pazi, Amesema sasa katika mkoa wa Dar es Salaam hakutakuwa na utata tena wakati wa Uchaguzi na hakutakuwa na watu watakao gushing umri kwa kutaka nafasi za madaraka maana mfumo huu hautaruhusu hayo.

Chanzo: bongo5.com