Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tundu Lissu awapaka matope Kikwete na Mkapa

Lissu Pic Tundu Lissu awapaka matope Kikwete na Mkapa.

Sat, 29 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu Lissu ‘amewatusi’ Marais wastaafu, Hayati Benjami William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwaita wezi walioshiriki kuiba mali za umma katika utawala wao.

Akizungumza katika Mkutano wao uliofanyika Bukoba, Mkoani Kagera, Lissu alisema enzi za utawala wao kulifanyika matukio ya wizi na wao wakiwa ni marais wa nchi nq kudai jambo hilo linapaswa kukosolewa bila kujali imani zao na mchango wao katika Taifa.

Shida ya Maji: Tunawakosea Watanzania – DUWASAMajaliwa awakaribisha Wawekezaji sekta ya Mbolea

Amesema, “Tuyazungumze haya majimboni kwetu na tujipange kulinda vya kwetu, kwa sababu mimi nilimsema Rais Mkapa kwa wizi wake na akanikamata na kukaa na kesi miaka sita ingawa Mkapa alikuwa mkatoliki kama mimi lakini yeye alikuwa mwizi japo alitembea na limsalaba lake.”

“Sio Mkapa tu, hata huyu naye ni wale wale wezi walioibia nchi yetu na  Tegeta Escrow bila kusahau maujambazi mengine aliyofanya katika kipindi cha utawala wake na maujambazi mengine ambapo nilipomsema alinifungulia kesi tatu,” amebainisha Tundu Lissu.

Hata hivyo, Lissu alitumia muda mwingi kuongea lugha za kuwakashifu Viongozi hao na chama hicho kikuu cha Upinzani CHADEMA, kimeonekana kukosa uungwaji mkono na mikutano yao kukosa wahudhuriaji wengi kama ilivyotokea kwenye Mkutano uliofanyika hivi karibuni, Temeke jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live