Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tundu Lissu amjibu Kinana

Lissu PicRGTHHH Tundu Lissu amjibu Kinana

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Tundu Lissu, amesema mazungumzo ya maridhiano kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chadema yamevunjika kutokana na CCM kutokubali mapendekezo yao hususan madai ya upatikanaji katiba mpya.

Akizungumza nasi, jana tarehe 6 Februari 2024 kwa njia ya simu, Lissu amesema si kweli kwamba mazungumzo hayo yamevunjika kutokana na Chadema kutumia kauli za udhalilishaji katika mikutano yake ya hadhara.

Lissu ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, kusema mazungumzo hayo yamevunjika baada ya Chadema kutumia mikutano ya hadhara kukashifu na kudhalilisha viongozi wa Serikali hasa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Hilo la kumdhalilisha Rais halijawahi kuwa hoja ya mazungumzo ya maridhiano. Tulichokizungumzia na walichokikataa ni mabadiliko ya Katiba na mfumo mpya wa uchaguzi. Hatujawahi kuzungumzia kauli na msimamo wetu kuhusu Rais Samia na utendaji kazi wake. Wanataka kubadilisha ‘narrative’, amesema Lissu na kuongeza:

“Suala sio kutuita tena kwenye meza ya mazungumzo. Suala ni je, wako tayari kukubaliana na mapendekezo yetu juu ya Katiba Mpya na mfumo mpya wa uchaguzi? Kama hawako tayari kufanya hivyo, mazungumzo hayatakuwa na maana yoyote.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live