Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tundu Lissu: Nitakuwepo kushiriki maandamano

Mbowe Lissu Cdm Cdm Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Sat, 20 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) – Bara, Tundu Lissu ametangaza kushiriki maandamano ya amani yaliyoitishwa hivi karibuni na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mbowe alitangaza maandamano hayo yatakayofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 24 Januari mwaka huu kuishinikiza Serikali kuzingatia maoni na mapendekezo ya wadau wa uchaguzi nchini.

Akizungumza na Watanzania kwa njia ya mtandao leo Jumamosi kutokea jijini Abidjan nchini Ivory Coast kunakofanyika fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON), Lissu alisema mbali na kuwepo jijini humo kuiunga mkono Timu ya Taifa (Taifa Star) masuala ya siasa ya Tanzania ni muhimu.

“Mimi nitakuwepo Dar es Salaam nitashiriki maandamano ya amani ya siku ya tarehe 24 ya wiki ijayo lakini hili haliwezi kuwa jukumu langu au la Mbowe peke yake au Chaderma peke yao kwa sababu katiba bora mpya na mfumo bora wa uchaguzi vinatuhusu sisi wote.

“Hivyo naomba kila mmoja wetu ajitafakari na atafakari katika mapambano haya na katika ustawi wa Taifa letu… natoa rai kwa wananchi wa Tanzania na wenye nia njema na nchi yetu nao wawepo Dar es Salaam siku hiyo ya kihistoria ili nao washiriki katika maandamano haya ya amani,” amesema Lissu.

Lissu amesema katika wa miswada mitatu iliyopelekwa bungeni Novemba mwaka jana ni wazi CCM haitaki kufanya mabadiliko yoyote ya maana kwa mfumo wa katiba na uchaguzi.

“Hata baada ya mazungumzo ya mwaka jana, Rais Samia Suluhu Hassan licha ya ahadi zake nyingi ndani na nje ya Tanzania, amekataa maridhiano ya kisiasa ambayo yangeondoa nchi kwenye kivuli cha utawala wa kiimla wa chama kimoja na madhara yake yote kwa nchi yetu,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live