Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tulia afunguka kuhusu mgawanyo wa jimbo

Spika Tulia Ahutubia Mkutano Wa 146 Umoja Wa Mabunge Duniani Tulia afunguka kuhusu mgawanyo wa jimbo

Thu, 4 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spika wa Bunge, Tulia Ackson amesema iwapo serikali itaridhia mchakatao wa kuligawa jimbo la Mbeya Mjini lenye kata 36, basi ujikite katika kuwasogezea wananchi huduma badala ya kuangalia idadi ya kata.

“Kwa jiografia la jimbo la Mbeya mjini kuna bonde la Uyole ni kama vile maaeno yapo mawili, sasa kuna watu wa Uyole na wengine wa upande wa mjini. Ukiligawanya kata zilizopo bonde la Uyole zitaingia Uyole, zilizopo mjini zitaingia Mjini,” amesema Dk Tulia katika mahojiano maalumu na runinga moja nchini.

Katika mahojiano hayo yalkifanyika katika makazi yake leo Alhamisi Mei 3,2023 Jijini Dodoma, Dk Tulia amefafanua kuwa Mbeya mjini haijanyooka kama Morogoro bali ipo kama bakuli kutokana na kuzungukwa na milima.

Hivyo basi, Spika amefafanua kuwa namna bora ya kuligawa ni kuhakikisha watu wanansogezewa huduma badala ya kuzifuata.

“Ningependa ligawanywe kwa watu kuwasogezea huduma, mfano watu wa Mjini; wahudumiwe mjini na wale wa Uyole, pia wahudumiwe Uyole ili kupunguza umbali,” amesema Dk Tulia ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini kwa sasa.

Aitha, Dk Tulia amesema ikitokea Mbeya Mjini ikagawanywa na kuwa majimbo mawili, basi jimbo la Uyole litakuwa na kata chache kijiografia japo litakuwa na eneo kubwa na kwamba kata 14 zitaingia Uyole na 22 zitabaki Mbeya Mjini.

Hata hivyo, Dk Tulia amesema suala la kugawa jimbo la Mbeya Mjini sio jipya, kwa sababu hayati Rais John Magufuli alivyopita Mbeya Mjini wakati wa kampeni aliwaahidi wananchi.

Dk Tulia alisema hayati Magufuli aliwaambia wananchi kwamba endapo wangechagua Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika kata zote 36 na mbunge, basi jimbo hilo lingegawanywa. Na kwamba kwa kuwa ahadi hiyo ilitokana na uchaguzi wa 2020, hivyo michakato yake iliishaanza.

“Sio jambo jipya kwamba watu wanashtuka sasa hivi, kama vile ni jambo la ajabu hapana. Michakato ilishaanza, vikao vya halmashauri, kisha baraza la ushauri la wilaya na baraza la ushauri la mkoa,” amefanunua Spika Tulia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live