Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tulia acharuka "Waitara amelivunjia heshima Bunge na Spika"

Tulia Waitara Waitara.png Spika Tulia ampa onyo Mbunge Mwita Waitara

Tue, 14 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amempa onyo kali Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara kwa kukiuka maamuzi ya Bunge pamoja na Spika kuhusu hoja aliyoiwasilisha Bungeni juu ya uvamizi wa wanyamapori kwenye makazi ya watu ambao hupelekea vifo kwa wananchi.

Akizunguma Bungeni Jijini Dodoma leo Juni 14, 2022 Spika amesema kuwa Mbunge huyo amepuuza maamuzi yaliyofanywa na Bunge yaliyoridhia kufanyika kwa uchunguzi juu ya hoja hiyo aliyoitoa Bungeni hapo wakati wa uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara ya Utalii na Maliasili.

Waitara anadaiwa kufanya mahojiano na kituo cha habari kimoja nchini na kutoa matamshi yakutokuwa na imani na kitendo cha Serikali kujichunguza katika sakata hilo huku akimtaja Spika Tulia kuwa anafahamu vyema kuhusu masuala ya kisheria kwani alishawahi kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akieleza hilo Spika Tulia amesema kuwa Mbunge huyo amefanya kosa kwani tayari Bunge lilitoa maamuzi ya kufuatilia kwa kina sakata hilo na kuwa kitendo hicho kinamvunjia heshima yeye kama Spika pamoja na Bunge.

" Mbunge Mwita Waitara anapaswa ajue kuwa najua utaratibu kuliko anavyojua yeye, na sio hivyo tu nazijua hizo sheria vizuri kuliko anavyzoijua yeye"

"Mtu mwenye afya ya akili vizuri alipaswa kufikiria maamuzi ya Bunge yaliyotolewa hapa"

"Mbunge Mwita Waitara amekiuka sheria na taratibu za Bunge na hili halikubaliki, kuivunjia heshima Bunge wala Spika"

" Nampa onyo, asirudie tena kitendo hicho cha kudharau maamuzi ya Spika na Bunge, baada ya kumpa onyo hilo nimemsamehe" Amesema Spika Tulia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live