Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tukitambua malengo ya Rais Samia kila kitu safi -Shaka

Shakavvvf Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamidu Shaka

Wed, 1 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Mapinduzi (CCM ) kimesema iwapo kila Mtanzania atawajibika na kufanya kazi kama yalivyo malengo, mipango na mikakati ya Rais Samia Suluhu Hassan, Tanzania itapaa na kuwa nchi yenye uchumi unaojitegemea.

Pia, kimesema kuwa kauli mbiu ya Kazi Iendelee ina maana kwamba, kila mtu anayeishi mjini na kijijini anapaswa kutambua wajibu wa kujituma, kufanya kazi na kuitumikia nchi yake ipasavyo.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu wa NEC Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Kariakoo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Amesema iwapo kila Mtanzania atayaweka malengo ya kisera na kimkakati ya Serikali na namna inavyotaka wananchi kujituma na kufanya kazi kwa bidi, basi kila kitu kitakwenda vizuri.

"Binadamu anapoamini kufanya kazi ni kama adhabu au utumwa huo ni mtazamo hasi usiofaa kufuatwa, kama Watanzania tunapaswa tunachapa kazi ipasavyo kwenda sambamba na kauli mbiu ya Rais Samia ya Kazi iendelee," amesema Shaka.

Amesema katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Samia ameakisi mambo yaliyokuwa yakitamaniwa na jamii yatokee.

"Tulipopata uhuru na kufuzu Mapinduzi ya Zanzibar, kaulimbiu za viongozi wetu na waasisi wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume, inamtaka kila mtu afanye kazi, ikaelezwa kazi ni kipimo na thamani ya utu wa mtu," amesema Shaka na kuongeza:

"Tafsiri ya uhuru ni kufanya kazi, watu walishiriki kwa pamoja kufanya kazi za maendeleo, leo hii Rais Samia anaendeleza maono ya waasisi wetu hasa katika suala la uchumi wa kipato kwa Watanzania."

Katika hatua nyingine, Shaka amesema CCM inaridhishwa jinsi wananchi wanavyoshiriki kwenye shughuli za uzalishaji mali na kuipongeza Serikali ya Rais Samia kwa kuendelea kuboresha huduma za kijamii na miundombinu ya kiuchumi ili kuharakisha maendeleo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao hicho, viongozi wa jumuiya hiyo wamesema wako tayari kushirikiana bega kwa began a Serikali katika kukuza uchumi wa Taifa.

Mwenyekiti wa umoja huo, Martin Masawe amesema wanaamini kuwa mahusiano mazuri na Serikali pamoja na CCM, yatatengeneza misingi mizuri ya ushirikiano utakaorahisisha utatuzi wa changamoto mbalimbali.

“Tuna imani na Serikali ya Rais Samia kwa kuwa inaendelea kujipambanua katika kuboresha mazingira bora kwa wafanyabiashara wa ndani, hivyo tunaamini iwapo tutaendelea kuwa karibu, hata zinapotokea changamoto ni rahisi kupatiwa ufumbuzi,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live