Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tisa Kugombea Uspika

Katibu Wa Bungezzz.png Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma leo kuhusu kukamilika kwa zoezi la uteuzi na utaratibu wa Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Katibu wa Bunge hadi kufikia leo saa Kumi Jioni Majina ya jumla ya Wagombea Tisa (9) yalikuwa yamewasilishwa na kukidhi matakwa ya kisheria kwa ajili ya uchaguzi wa Spika unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 1 Februari, 2022.

Aidha, Katibu wa Bunge amesema miongoni mwa Wagombea hao nane sio Wabunge na mmoja ni Mbunge.

Aliwataja magombea hao kuwa ni Abdulla Mohammed Said (NRA), Mhandisi Aivan Jackson Maganza (TLP), David Daud Mwaijolele (CCK), George Gabriel Bussungu (ADA -TEA), Kunje Ngombale Mwiru (SAU), Maimuna Said Kassim (ADC), Ndonge Said Ndonge (AAFP), Saidoun Abrahaman Khatib (DP) na Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live