Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu ya Bunge Tanzania yapokea vifaa kushiriki michuano ya Mabunge

C90C2004 7ECF 4F10 804A 3F81270CEC0C 660x400.jpeg Timu ya Bunge Tanzania yapokea vifaa kushiriki michuano ya Mabunge

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: millardayo.com

SportPesa leo imetoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kwa timu ya Bunge ambayoinatarajia kushiriki mashindano ya mabunge ya nchiwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mkoani Arusha.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa habari ofisi za Bunge kabla ya kuanza rasmi mashindano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Bodiya Wakurugenzi SportPesa na vile vile ni Mwenyekiti waBunge Sports Club Tarimba Abbas alianza kwa kuwashukuruSportPesa kwa udhamini wao ili kufanikisha ushiriki wamashindano hayo.

“Hii ni mara ya pili kwa SportPesa kutoa udhamini huoambapo mnamo mwaka 2017 walifanya hivyo kwenye mashindano ya Bunge “

“Tunapenda kuwahahakikishia mashabiki kuwa tunatarajiaushindi wa kishindo huku tukipeperusha  bendera ya Bunge la Tanzania”

“Tulikaa kikao na viongozi wa timu  na wamenihakikishiakwamba watafanya vizuri ili kuhakikisha wanarudi na ushindi”.

“SportPesa imedhamini kwa kutoa vifaa vya timu zote 8 ikiwemo Mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa pete, dart, kuvuta Kamba pamoja na michezo mingine ikiwemosare za viongozi”.

Kwa upande wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mwakilishi wa Katibu wa Bunge Mohammed Mwanga alianza kwa kuwashukuru SportPesa kwa uwapatiavifaa Bunge Sports Club na kuwaomba wabunge kuvitendeakazi.

“Nawatakia Kila la kheri kwenye mashindanoyatakayofanyika Karatu na Arusha, safari njema. Mcheze kwa ushikamano na kuhakikisha mnaondoka na ushindi”

Meneja Uhusiano na Mawasiliano SportPesa Sabrina Msuya aliwashukuru timu ya Bunge la Jamhuri kwa kujitoa na kuunda timu mbalimbali na kuwatakia kila la kheri kwenyemashindano hayo yatakayohusisha nchi za Afrika Mashariki.

Kwa niaba ya viongozi wa Bunge Sports Club Mama Salma Kikwete aliongeza kwa kuwashukuru SportPesa na kuombamashirika  mengine kuhamasika katika michezo na kusaidiakwenye mashindano mbalimbali. Pia aliwaomba wabungekuhakikisha wanashiriki kwa nidhamu na ushirikiano ili kuleta matokeo mazuri.

Chanzo: millardayo.com