Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tazama picha za matukio mbalimbali yaliyojiri bungeni leo May 8, 2018

7657 1 3 TZW

Wed, 9 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea leo Bungeni mjini Dodoma, likiwa limeongozwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai. Tazama picha za Wabunge mbalimbali wakiwa katika kipindi cha maswali na majibu



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisisitiza jambo leo Bungeni Jijini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu



Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii Mhe. Japhet Hasunga Akitoa maelezo kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa migogogoro ya mipaka kati ya hifadhi za Taifa na wananchi inapatiwa ufumbuzi leo Bungeni Jijini Dodoma

Mbunge wa kuteuliwa ( CCM) Mhe. Anne Kilango Malecela akisisitiza kuhusu Serikali kuweka mikakati ya kuimarisha miundo mbinu ya barabara katika jimbo la Same ili kusaidia kukza uzalishaji wa mazao ya biashasra leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma leo



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akitoa maelezo Bungeni kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwalipa fidia askari na wapiganaji wanaoathirika wakati wanatekeleza majukumu ya kulinda usalama ndani na nje ya nchi kwenye vyombo vya Umoja wa Mataifa (UN) au SADC leo Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu



Sehemu ya wageni waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma



Mbunge wa Geita Mhe. Msukuma Joseph Kasheku akiuliza swali Bungeni leo Jijini Dodoma kuhusu ni lini Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) utawasilisha bajeti yake ya kuhudumia jamii katika Baraza la Madiwani wa Geita ili waweze kuangalia vipaumbele vyao na kuwapa vipaumbele vya Halmashauri hiyo



Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akieleza mikakati ya Serikali kuwawezesha wachimbaji wadogo katika maeneo yote nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma leo

Loading...
Chanzo: bongo5.com