Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tazama matukio katika picha kutoka Bungeni leo – May 31, 2018

8517 1 9 TZW

Fri, 1 Jun 2018 Chanzo: bongo5.com

Kikao cha 41, mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea Jijini Dodoma, Leo Bunge limeongozwa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge.Kipindi cha Maswali na Majibu kiliendelea na wabunge walijibiwa na Serikali



Waziri wa Madini, Angellah Kairuki akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/2019 leo Bungeni Jijini Dodoma



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama akitoa maelezo Bungeni kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali katika kuwalinda watoto wa kike



Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kupambana na Janga la Ukimwi hapa nchini ikiwemo kuhamasisha upimaji wa Virusi vya UKIMWI hasa kwa wanaume kote nchini ili wajue hali zao na kuchukua hatua stahiki



Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo (wa kwanza kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini,Angellah Kairuki Bungeni Jijini Dodoma leo



Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula aliyesimama (kushoto) na Mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo Prof. Abdulkarim Mruma wakitambulishwa Bungeni leo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.



Sehemu ya Viongozi wa Tume ya Madini na wageni mbalimbali wakiwemo wakuu wa Mikoa yenye madini wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Bungeni Jijini Dodoma leo



Sehemu ya Wanafunzi waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu

( Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

Loading...
Chanzo: bongo5.com