Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tatizo la ajira Tanzania latawala mdahalo wa Vijana ACT- Wazalendo

98314 Pic+ajira Tatizo la ajira Tanzania latawala mdahalo wa Vijana ACT- Wazalendo

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baadhi ya wagombea  wa uenyekiti wa ngome ya vijana wa chama cha siasa nchini Tanzania cha ACT Wazalendo wametaja tatizo la ajira kwa vijana kuwa kipaumbele chao endapo watachaguliwa kuongoza ngome hiyo.

Wagombea hao sita wamejinadi leo Jumamosi Machi 7,2020 katika mdahalo huo uliofanyika Sinza Dar es Salaam ambapo uchaguzi wake utafanyika Machi 9, 2020 jijini Dar es Salaam.

Julius Masabo amesema kati ya vijana 800,000 wanaomaliza shule kila mwaka ni asilimia tano  tu wanaopata ajira.

"Sisi vijana tunadai haki yetu tupewe. Haki huwa haiombwi, huwa inadaiwa.

Kuna gharama za kudai haki, lakini nitapambana kupata haki ya ajira," amesema Masabo.

Naye Kudra Abbas ambaye ni katibu wa vijana, Ofisa tafiti makao makuu ya chama hicho amesema kuna tatizo la kutoheshimu haki za vijana nchini.

Pia Soma

Advertisement
"Asilimia 70 ya wananchi ni vijana. Kila mwaka kuna vijana 1.2 milioni wanaomaliza vyuo vikuu na taasisi. Lakini wengi hawaajiriwa," amesema Abbas.

"Ndani ya miezi sita nitaingiza wapiga kura 1.5 milioni. Nitapigania mikopo kwa wanafunzi, nikishindwa nitajiuzulu. Nitaanzisha ASF - ACT Wazalendo Students Org ili kuwasaidia wanafunzi," amesema.

Hamza Gere anayegombea nafasi hiyo pia amesema atapigania haki ya vijana kuajiriwa hasa kwa vijana wanaoishi vijijini.

"Vijana wanaoishi vijijini ni zaidi ya asilimia 50, mijini asilimia 30. Hao ndio wanaotafuta ajira," amesema Gere.

Amesema atawapigania wasichana wanaokatazwa kuendelea na masomo baada ya kupata mimba akisema wana haki ya kupata elimu.

Kuhusu uvunjaji wa haki za binadamu amesema ataongoza mapambano ya kutetea haki za binadamu.

"Bara kuna watu wasiojulikana, Zanzibar kuna mazombie. Nitaendesha mapambano ya kutetea haki za binadamu."

Kwa upande wake, Winston Moga amesema atarekebisha muundo wa ngome hiyo ili kuwa na utendaji mzuri tangu ngazi za wilaya, mikoani na Taifa.

Amesema pia atahakikisha ngome hiyo inakuwa na vyanzo vyake vya mapato.

Mgombea mwingine ni Abdul Nondo ambaye ametaja vipaumbele viwili kati ya 10 akisema ataendeleza mapambano ya demokrasia na kuongeza wanachama wa ACT Wazalendo.

"Nitajenga ngome ya vijana kuwa ya kitaifa siyo kwa Dar es Salaam pekee. Pia nitaifanya ngome kuwa mtetezi wa vijana," amesema Nondo.

Nondo aliyepitia misukosuko ya kufunguliwa kesi kwa madai ya kujiteka mwaka 2018, amesema ataendelea kupigania mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Hoja ya ajira kwa vijana pia ilizungumzwa na Julius Masalo akisema tatizo hilo linasababishwa na sheria kandamizi.

"Leo waandishi wa habari wanahitaji kuwa na Sh1 milioni ili kufungua blog. Tunahitaji kupigania haki ya kuwasiliana na kuwawezesha vijana kupata ajira," amesema

Chanzo: mwananchi.co.tz