Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tarimba aahidi maendeleo lukuki kinondoni

D8b86f57c60687405f14341a4ec37115 Tarimba aahidi maendeleo lukuki kinondoni

Mon, 19 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA ubunge katika jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abbas Tarimba amewataka wakazi wa Kinondoni kumpa nafasi ya kuwa mbunge wao pamoja na Rais John Magufuli na watalipa hisani hiyo kwa kuwaletea maendeleo lukuki.

Aidha, amewaahidi wakazi wa jimbo hilo kumaliza matatizo yao makubwa ikiwemo ajira kwa vijana, kutoa mikopo kwa kila mtu, kuboresha huduma za afya lakini pia kujenga shule mbili za kidato cha tano na sita.

Tarimba aliyasema hayo wakati akiwa kwenye mikutano ya kampeni katika maeneo ya Kigogo na Hananasif Kinondoni jijini Dar es Salaam.

“Watu wa Kinondoni tarehe 28(Oktoba) mtupatie kura mimi pamoja na Rais John Pombe Magufuli cha kuwalipa hisani yenu ni kuwaletea maendeleo lukuki kwa hisani ya kura zenu. Kigogo mlikuwa mnatafuta majawabu ya matatizo yenu na jibu hilo ni Mimi nitumeni mimi nikawakilishe mawazo yenu,” alisema.

Alisema katika mikopo inayotolewa na halmashauri kwa vijana, kuna kigezo kilichowekwa kwa vijana wanaostahili kupata mikopo hiyo umri wao usizidi miaka 35, kigezo alichokielezea kuwa hakina afya.

“Kwani waliozidi umri wa miaka 35 hawapaswi kupata mikopo? Tutakwenda kulishughulikia ili mikopo iwe kwa wote wenye sifa ya kupata mkopo. Ni kweli Vijana wana mahitaji ya mikopo lakini je walio zaidi ya miaka 35 wao hawastahili? Hii ni hoja nitakwenda nayo kuwashawishi wote wenye sifa na vigezo wapate mikopo nafuu ya halmashauri zetu,” alisema.

Alisema kwa upande wa elimu atahakikisha shule mbili za kidato cha tano na sita zinajengwa kwa kuwa elimu ndio msingi wa maisha. Pia aliahidi kumalizia shule zote zilizoanza kujengwa jimboni humo.

Hivi karibuni, akizungumza katika mkutano wa kampeni ya mgombea urais wa chama hicho, Rais Magufuli, alimshukuru kiongozi huyo kwa kuwajengea wakazi wa Kinondoni masoko mawili makubwa Tandale lililogharimu Sh bilioni nane na Magomeni Sh bilioni 8.9.

Chanzo: habarileo.co.tz