Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamko la Baraza la Wazee CHADEMA kuhusu vitendo vya polisi

WAZEE CHADEAMAAAAA Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee CHADEMA, Roderick Lutembeka

Tue, 17 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Wazee wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, limelaani kitendo cha jeshi la Polisi kilichofanyika jumapili ya tarehe 15/08/2021 cha kukamatwa kwa wanachama na viongozi wapato 20 walikuwa kwenye Parokia ya Kawemo jijini mwanza.

Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Roderick Lutembeka, wamesema kitendo hicho si cha kiungwana, na kuwa hakukuwa na sababu yoyote ya kuwakamata viongozi au wanachama hao.

“Tunalaani kitendo kilichofanyika jumapili ya tarehe 15/08/2021 huko Mwanza ambao Jeshi la Polisi liliwakamata Wanachama na Viongozi wapatao 20 walipokuwa katika maeneo ya kanisa kwenye Parokia ya Roman Catholic Kawekamo Mwanza”

“Jambo hili limetokea zikiwa ni siku chache likiwa limetokea tena huko Mbeya na kufuatiwa na kukemewa na Katibu Mkuu wa TEC aliyeweza kuitolea ufafanuzina kusema kwamba haikuwepo sababu yoyote ya kuwakamata Viongozi au Wanachama waliokuwa wamevaa sare”

Waliongeza kusema kuwa vitendo hivyo ni vya uonevu na kwamba vinakiuka haki za binadamu sambamba na kuibua chuki na uhasama usio na mantiki.

“Vitendo hivi vya uonevu, dhuluma, vitisho na ubaguzi si tu kwamba vinakiuka haki za watu zilizoainishwa katika Katiba ya JMT ibara ya 12 na 13 lakini vinaibua chuki na vinaweza kusababisha uhasama na kuhatarisha usalama”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live