Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takururu yaonya wagombea CCM

Cb63d46dcdf4e288b0ed60bffa644bec Takururu yaonya wagombea CCM

Thu, 4 Aug 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Iringa imetoa onyo kwa wagombea na wapiga kura wa chaguzi za Chama cha Mapinduzi (CCM) zinazoendelea, ikiwataka wao pamoja na mawakala wao kutojihusisha na rushwa.

Imesema katika robo ya Julai hadi Septemba, mwaka huu imeimarisha zaidi juhudi zake za kuzuia na kupambana na rushwa kwa kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kuzuia vitendo vyote vya rushwa.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake katika robo ya April hadi Juni 2022, Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Bahati Haule alisema; “Tunaendelea kuwasihi wananchi kufuatilia elimu tunazotoa na watuletee malalamiko yanayoangukia kwenye sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ili tuweze kuchukua hatua stahiki.”

Haule alisema taasisi hiyo itaendelea pia kufuatilia makusanyo ya serikali, uwasilishaji wa mapato na usimamizi wa rasilimali za umma na kuchukua hatua stahiki kwa wale watakaobainika kuzifuja.

Katika robo hiyo ya April hadi Juni alisema, taasisi yao ilipokea malalamiko 46 ambayo kati yake 18 yalihusu rushwa na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria kwa kuanzisha uchunguzi.

Huku ikishinda mashauri matatu yaliyoamuriwa na mahakama katika kipindi hicho, alisema walifungua mashauri mapya mawili na kufanya jumla ya kesi zinazoendelea kufikia 10.

Aidha alisema Takukuru Mkoa wa Iringa iliingilia kati utekelezaji wa miradi ya uchimbaji visima tisa katika halmashauri ya wilaya ya Mufindi yenye thamani ya Sh Milioni 358 hatua iliyowezesha mkandarasi wake (hakutajwa) kuondolewa baada ya kubainika hana uwezo wa kufanya kazi hiyo na kwa ubora unaotakiwa.

“Kwa ujumla katika robo hiyo tumefuatilia utekelezaji wa miradi 13 yenye thamani ya Sh Bilioni 6.9 katika sekta za afya, barabara na maji,” alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz