Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taarifa mpya kwa wagombea waliokatwa na Wasimamizi wa uchaguzi

Maxresdefault 2 660x400 1 Taarifa mpya kwa wagombea waliokatwa na Wasimamizi wa uchaguzi

Thu, 27 Aug 2020 Chanzo: millardayo.com

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imewataka wagombea ambao hawajateuliwa kuomba maelezo kwa wasimamizi wa uchaguzi juu ya kutokuteuliwa kwao kwani Tume ipo tayari kushirikiana nao.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera amesema Tume inashirikiana na umma ili kuhakikisha uchaguzi huu unakuwa wa huru na haki.

“Mtu ukiona hujateuliwa ni vizuri uulize kwa msimamizi wa uchaguzi akuelezee yeye ni kwanini na sisi Tume tuko tayari kushirikiana na nyinyi ili kuhakikisha uchaguzi huu unakuwa wa huru na wa haki “ Mahera.

“Huwezi ukakata mtu kwa matakwa yako kwa sababu Tume ya Taifa inafanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni, tumeweka sifa za wagombea kwa ngazi zote, Madiwani, Wabunge na Rais, lakini tumeweka masharti ya uteuzi, mtu ukimuona hajateuliwa maanake hajatekeleza yale masharti” Mahera

RAIS MAGUFULI AAMURU MAGARI 130 YA KIFAHARI YALIYOTAIFISHWA YAGAWANYE MIKOANI

Chanzo: millardayo.com