Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TLP NA UDP WASITISHA KUMUUNGA MKONO JPM

Naivu 1?fit=417%2C422 TLP NA UDP WASITISHA KUMUUNGA MKONO JPM

Wed, 7 Oct 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania imesema Vyama vya TLP na UDP vilisitisha mpango wa kumuunga mkono Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Magufuli kwasababu havikufuata Kanuni na Sheria za Uchaguzi.

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza amesema, waliwaambia TLP na UDP suala hilo lina utaratibu ambao walitakiwa kuufuata, na walipoona hawajafuata Vyama hivyo vimekaa kimya na havisikiki tena

Ameongeza, UDP wameendelea na kazi zao za kampeni, wakiwa na Mgombea wao na wanatangaza Sera za Chama chao. Aidha, TLP ambao waliweka mabango wameyatoa na wanaendelea na kampeni zao

Nyahoza amesema, “Kwa hiyo Vyama ni sikivu, vile ambavyo sio sikivu wawe wasikivu na kuzingatia Sheria na Kanuni maana kama Mgombea wa Chama chako asipokuwa msikivu, akishinda kwenye Uchaguzi itakuwaje?”

Chanzo: zanzibar24.co.tz