Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF yabadili viingilio vya mechi ya watani Yanga na Simba

97837 Kiingilio+pic TFF yabadili viingilio vya mechi ya watani Yanga na Simba

Wed, 4 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limebadilisha viingilio vya mchezo wa Yanga dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Machi 8, 2020 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Afisa habari wa Shirikisho hilo, Clifford Ndimbo, alitangaza mabadiliko hayo ni katika sehemu ya VIP B na C kwa Sh20000 huku awali ilikuwa ni Sh 15000.

Ndimbo alisema katika upande mwingine wa viti vya rangi ya machungwa ni Sh 10,000 na viti vya rangi ya bluu na kijani sh 70,000.

Viingilio kwa ujumla ni 30,000, VIP B &C 20,000, viti vya rangi ya machungwa 10,000 na vya rangi ya bluu na kijani 70,000.

Tiketi za mchezo huo zimeanza kuuzwa katika vituo mbalimbali, huku siku ya mchezo hakutokuwa na uuzwaji wa tiketi katika eneo la uwanjani.

Chanzo: mwananchi.co.tz