Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TCD yazindua jukwaa la wanawake

Lipumbaaapic Data TCD yazindua jukwaa la wanawake

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), leo kimezindua rasmi Jukwaa la Wanawake na wadau wa demokrasia nchini kwa lengo la kuongeza nguvu ya ushiriki wao kwenye siasa pamoja na kuwajengea uwezo wa kiuongozi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwa hilo, Mwenyekiti wa TCD Prof. Ibrahim Lipumba amesema litatumika kuleta usawa katika siasa na uongiozi.

Prof. Lipumba wanawake wanasiasa wa vyama mbalimbali kulitumia kupaza sauti zao kwa pamoja juu ya masuala ya sheria, changamoto ambazo zimekuwa kikwazo kwao kushiriki chaguzi mbalimbali pamoja na masuala ya jinsia.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na Balozi wa Marekani nchini, Michael Battle na Balozi wa Uswisi nchini Didier Chassot, ambao walisema wameona nia safi ya Rais Samia Suluhu Hassan kudumisha demokrasia nchini. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live