Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Diwani wa CCM afariki dunia

Diwani Pic Data Diwani wa CCM afariki dunia

Sun, 15 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diwani wa Kata ya Mianjani (CCM) jijini Tanga, Yakub Nuru Othman amefariki dunia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Abdulrahman Shiloo leo Jumapili Mei 15, 2022 diwani huyo amefariki jijini Dar es Salaam alikokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba mwili wake unatajariwa kusafirishwa leo kuelekea jijini Tanga na kwamba mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho nyumbani kwake katika Kata ya Miayanjani.

Yakubu aliingia kweenye nafasi hiyo ya udiwani baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2020.

Akimzungumzia marehemu baada ya kupokea taarifa za msiba huo, Diwani wa Viti Maalumu, Mayungi Daruweshi amesema walishirikiana vizuri na marehemu katika Baraza la Madiwani na kwamba alikuwa mchapa kazi na mwenye hekima.

"Mzee Yakub alikuwa na hekima na sote tulimtumia hasa tulipohitaji busara zake hakusita kutusikiliza na kutushauri vyema na alikuwa mwenyekiti wa kamati ya maadili, hakika tumempoteza mtu muhimu na mwenye weledi," amesema.

Mkazi wa kata ya Miyanjani, Musa Kipingu amesema wananchi wamempoteza kiongozi waliyempenda na kumuamini kwa kuwa aliwatumikia vizuri kwa kuzitatua kero zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live