Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAMISEMI yaomba Sh8.77 trilioni

Bajetipiic Data Bashungwa amewasilisha bajeti ya TAMISEMI leo

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imeomba kuidhinishiwa na Bunge Sh8.77 trilioni kwa mwaka wa bajeti 2022/2023.

Waziri wa Tamisemi,  Innocent Bashungwa ameomba bajeti hiyo leo Alhamis Aprili 14, 2022 ambapo amesema kati ya fedha hizo Sh5.51 trilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida yanayojumuisha mishahara Sh4.62 trilioni na Sh884.86 bilioni kwa ajili ya matumizi mengineyo.

Aidha, Bashungwa amesema kati ya maombi hayo Sh3.27 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo kati ya fedha hizo Sh2.15 trilioni ni fedha za ndani na Sh1.12 trilioni ni fedha za nje.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live