Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye amewataka wanansiasa wote nchini kuacha kutumia kipindi cha uchaguzi kuingilia na kuharibu mshikamano uliopo kati ya wananchi na Serikali.
Sumaye amesema baadhi ya wanasiasa husababisha hali hiyo na kukwamisha maendeleo kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kujitoa kwa michango mbalimbali inayoanzishwa na Serikali.
"Muda mchache kabla ya kufika uchaguzi kila diwani hutaka jambo ambalo haliwezekani lifanyike na kuona watumishi wa Serikali hasa mkurugenzi anawarudisha nyuma na kuzua mizozo," amesema Sumaye.
Amesema kipindi cha uchaguzi wanasiasa wamekuwa wakiingilia na kukwamisha mipango mbalimbali ya Serikali na kurudisha nyuma muamko wa wananchi kujitoa kuchangia maendeleo yao.