Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sumaye asema Waitara amewadharau wana Ukonga

13886 Sumaye+pic TanzaniaWeb

Sat, 25 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, amesema Mwita Waitara aliyehama Chadema na kuhamia CCM, amewadharau wana Ukonga.

Sumaye ameyasema hayo leo Agosti 25 katika uzinduzi wa kampeni za Chadema, jimbo la Ukonga.

Asia Msangi, ndiye mgombea ubunge jimbo hilo kupitia Chadema katika uchaguzi utakaofanyika Septemba 16.

“Waitara alikuwa mbunge, leo anazungumza habari za Mbowe. Mbowe ndiyo alimchagua kuwa mbunge? Waitara amewadharau sana, amewadharau wana Ukonga kupita kiasi,” amesema.

“Kwanini mtu afanye madharau ya namna hii na sisi tutake kumfikiria? Haya machama yanayojidai yameleta uhuru yana kiburi hujawahi kuona,” ameongeza

Sumaye ambaye ni mjumbe wa Kamati kuu Ya chama hicho, amesema nchi zote zenye maendeleo ni zile ambazo zimeondoa vyama kongwe.

Kadhalika amesema iwapo nchi haina demokrasia ya kweli ya vyama vingi basi taifa litakuwa na wanyonge, na maskini.

“Sisi wengine tumetoka CCM kule ndio kulikuwa na makulaji, kila kitu kipo safi lakini nikasema raha yangu iko wapi kama watanzania wanateseka. Lazima maslahi ya umma yawe mbele kuliko maslahi binafsi,” amesema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz