Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sumaye akemea makada wa CCM wanaojali maslahi yao binafsi

Sumayeepic Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye

Sat, 5 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amewataka viongozi wa CCM kutowakubali makada wanaopigania maslahi ya makundi yao binafsi kwenye chama hicho.

Akizungumza mjini Babati mkoani Manyara, kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa chama hicho Sumaye, amesema baadhi ya makada wa chama wenye kujali maslahi yao wanajipanga kuweka makundi yao kwenye uchaguzi wa chama hicho.

Amesema viongozi hawapaswi kupanga safu zao na makundi kwenye uchaguzi wa chama ila wachaguliwe viongozi wa CCM watakaosaidia kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Amesema ni jambo zuri kwenye uchaguzi wa chama wa mwaka huu wawekwe watu ambao watatembea usiku na mchana kutafuta kura za CCM za mwaka 2025.

"Ni lazima CCM iunde timu za chama na siyo mtu binafsi kwani endapo watawafanyia mema wananchi hakutakuwa na ulazima wa kuwatetea wagombea," amesema Sumaye.

Amesema viongozi wanaotoa rushwa hawatakiwi kupewa nafasi ya kuongoza na wasipitishwe na chama kugombea nafasi zozote.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere amesema anafurahia kufanya kazi na viongozi wa CCM wa Mkoa huo kwani wanampa ushirikiano wa kutosha.

Naye Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Simon Lulu amesema chama hicho kinasherehekea miaka 45 kwa mafanikio makubwa.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz