Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sumaye: Watakaoshindwa kuvumilia uchaguzi Chadema wajitoe

86320 Sumayepic Sumaye: Watakaoshindwa kuvumilia uchaguzi Chadema wajitoe

Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pwani. Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye amewataka wagombea watakaoshindwa katika uchaguzi wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania kuwa kitu kimoja, watakaoshindwa kuvumilia wajitoe.

Waziri mkuu huyo mstaafu ametoa kauli hio leo Alhamisi Novemba 28, 2019 wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi Kanda ya Pwani unaofanyika Kibaha mkoani Pwani.

Amesema uchaguzi huo utakapomalizika watakaoshinda na watakaoshindwa wanatakiwa kushikana mikono kuhakikisha wanakuwa kitu kimoja.

"Kwenye timu ya watu wanne mshindi atapatikana mmoja na watatu watabaki kama huwezi kuvumilia inabidi ujitoe.”

"Hata mimi ninayegombea nina uhakika wa asilimia hamsini tu, kama ukikosa huwezi kuvumilia inabidi kukaa pembeni," amesema Sumaye.

Amesema majina yote yaliyorudi (kutoka kamati kuu) ni ya watu makini. Katika uchaguzi huo, Sumaye anawania wadhifa alionao sasa.

Wanaogombea makamu mwenyekiti ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita;  Mwenyekiti wa Mkoa wa Pwani, Baraka Mwago; mbunge wa Viti Maalum, Ruth Mollel na Diwani wa Majohe, Waziri Mwenevyale.

Katika nafasi ya mweka hazina majina yaliyopitishwa ni Florence Kasilima, Joseph Zahabu, Michael Mtally na Omar Mkama.

Chanzo: mwananchi.co.tz