Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sugu atinga mkutanoni na faili, afunguka

10148 Pic+sugu TanzaniaWeb

Sun, 5 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema),  Joseph Mbilinyi  maarufu Sugu leo Jumamosi Agosti 3, 2018 ametinga katika mkutano wa hadhara na faili lenye orodha ya ahadi mbalimbali alizozitekeleza tangu mwaka 2015.

Akizungumza leo jioni katika mkutano huo uliofanyika katika stendi ya Tukuyu-Uyole mjini hapa, Sugu amesema ameamua kufanya hivyo baada ya kuibuka maneno ya kumchafua kuwa hajafanya chochote tangu alipochaguliwa kuwa mbunge.

"Makamanda msishangae kuniona nimeshika faili mkononi. Nipo hapa kwa ajili ya kuwaeleza mambo niliyoyafanya tangu mliponichagua  maana kuna watu wanazunguka mitaani kunichafua kuwa sijafanya kitu" amesema Sugu.

Amesema  tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa mbunge mwaka 2010 hadi sasa amefanikiwa  kujenga madaraja zaidi ya 10 yanayounganisha jiji la Mbeya na Mbeya vijijini pamoja na kujenga maabara za kompyuta kila shule ya kata na kusomesha watoto yatima zaidi ya 400.

"Nimefanya vitu vingi lakini mimi sio mtu wa kiki eti  niwaite waandishi wa habari kwa kila kitu ninachokifanya  kama wapinzani wangu wanavyofanya,” amesema Sugu.

Chanzo: mwananchi.co.tz