Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sugu atangaza kuwania ubunge jimbo la Mbeya Mjini

SUGUUU WEB Sugu atangaza kuwania ubunge jimbo la Mbeya Mjini

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: Eatv

Aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu ametangaza nia yake ya kugombea tena ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi wa mwaka 2025.

Sugu amesema mara kadhaa baadhi ya wananchi wa Jiji la Mbeya wamekuwa wakimfuata kumuomba arejee nafasi ya ubunge wakidai mchango wake katika kuwasemea wameukumbuka.

"Bado naendelea kuishi mioyoni mwa wananchi wa Jimbo la Mbeya kutokana na mazuri niliyoyafanya kabla na baada ya nafasi yangu ya ubunge, nilifanya mengi kama vile ujenzi wa barabara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, maboresho katika sekta ya afya na kuwasaidia wajasiriamali aidha nimeendelea kuwasaidia wananchi wenye matatizo mbalimbali ambao hufika nyumbani," amesema Sugu.

Ameongeza; "Hata nikipita mitaani watu wanakimbilia kunilaki na kunisalimia huku wakisema wamenimiss nirudi tena ulingoni, nafarijika kuona bado wananipenda hivyo sitawaangusha bado nina influence kubwa kwa Taifa hili".

Amesema kwa miaka mitatu aliyokaa nje ya Bunge kitu kilichopungua kwake ni mshahara wa ubunge lakini maisha mengine yanaendelea ikiwemo biashara zake mbalimbali kama hoteli.  

Chanzo: Eatv