Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sugu: Mawaziri wamegeuka 'machawa' wa Mama, wananchi wamechoka

Sugu Samia Mnb Sugu: Mawaziri wamegeuka 'machawa' wa Mama, wananchi wamechoka

Sun, 11 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mbunge Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi (Sugu) akiwa kwenye Kongamano la CHADEMA Iringa jana, Desemba 10, 2022 amesema wao kama Upinzani wameamua kumshauri Rais juu ya masuala mbalimbali kwakuwa baadhi ya Mawaziri aliowateua wamegeuka kuwa Machawa badala ya kumsaidia.

“Nchi ipo vizuri, sisi kama Chama tupo vizuri zaidi ndio maana tunatoka na kumshauri Rais kwasababu Mawaziri aliowateua hawamsaidii kabisa katika kazi zake kwasababu wote wamegeuka na kuwa Machawa”

“Fanya vile vitu kwa standard na sio tu kukaa kusema Mama anaupiga mwingi ili tu Mama akusikie akuone na wewe unampigania, kumpigania Mama kama wewe ni Waziri ni kufanya kazi aliyokuteua kuifanya ipasavyo hapo mambo yanaweza kuwa sawasawa kwake”

“Mawaziri wamegeuka kuwa Machawa huku Wananchi wakiendelea kuchoka, Wananchi wamechoka sana, Mimi wananiita Taita ukipita utasikia ‘Taita hali ngumu sana Baba’, kwasababu hakuna anayetoa majibu ipasavyo kuhusu mambo yanayowakera Wananchi kuanzia suala la tozo,” amesema Sugu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live