Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stephen Masele Achukua fomu kugombea Uspika wa Bunge

AVvXsEjFAtwc7kLyuiI7aFoGmH8t3oxyUomQijla SvpNBSRwXlqU5gmbyT25Rrr ME12IHNFf5cut7Vu3ZJsIUQQjuTMsPGuQxm Stephen Masele Achukua fomu kugombea Uspika wa Bunge

Mon, 10 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Julius Masele leo Jumatatu Januari 10 amechukua Fomu ya kugombea Kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Masele ambaye amewahi kuwa Makamu wa Rais wa Kwa za wa Bunge la Afrika (PAP) amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Spika wa Bunge leo katika Ofisi za CCM Lumumba jijini Dar es salaam.

Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuanza mchakato wa kumsaka mrithi wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ambaye alijiuzulu tarehe 6 Januari mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana tarehe 9 Januari, 2022 Visiwani Zanzibar, Katibu wa NEC- Itikadi Uenezi CCM, Shaka Hamidu Shaka alisema mchakato huo utaanza kuanzia tarehe 10 hadi 30 Januari mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live