Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spika wa Bunge la Tanzania ataka viwango posho za madiwani viwekwe sawa

83023 Bunge+pic Spika wa Bunge la Tanzania ataka viwango posho za madiwani viwekwe sawa

Fri, 8 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.  Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema utaratibu wa kuwalipa posho madiwani kutoka katika halmashauri mbalimbali nchi, unachangia kuzua migogoro baina ya watendaji hao na viongozi wao.

Ndugai ameyasema hayo leo Novemba 5, 2019 baada ya Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mwita Waitara kujibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mpwapwa (CCM), George Lubeleje.

Akiuliza swali lake bungeni, Lubeje amesema mwaka 2000 hadi 2010 Serikali iliunda kamati kwa ajili ya kuangalia maslahi ya madiwani.

Amesema kamati hiyo ilikuja na mapendekezo kuwa madiwani waongezewe posho kulingana na majukumu yao.

“Unasema nini kuhusu kuongeza posho kwa madiwani pamoja na kuwalipa posho wenyeviti wa mitaa na vijiji,” alihoji mbunge huyo.

Akijibu swali hilo, Waitara amesema nia ya Serikali ikiwa na uwezo mkubwa, ni kuongeza posho kwa madiwani ili waweze kujikimu.

“Nchi hii tuna mitaa zaidi ya 4,200, tuna vijiji zaidi ya 12,000 na vitongoji zaidi ya 64,000 na kila mtaa ina wajumbe 6 na kila kijiji wajumbe 25 ni watu wengi kwelikweli ongeza madiwani,” amesema Witara.

Amewaomba madiwani kuendelea kufanya kazi na kwamba, uwezo ukipatikana wataongezewa posho.

“Nawaelekeza viongozi wa halmashauri wale madiwani wanaodai posho wasikopwe tena ili wachape kazi yao,” amesema.

Akizungumzia hilo, Spika Ndugai  amesema suala la posho za madiwani na wenyeviti wa mitaa na vijiji lina matatizo makubwa sana.

“Hii lugha ya kusema kuwa kila halmashauri ilipe kulingana na uwezo wake ni tatizo kubwa,” amesema.

Amehoji kwa nini kusiwe na mwongozo nchi nzima kwamba kipengele fulani malipo ni haya kwa Tanzania nzima.

“Hakuna cha uwezo wala nini? Malipo yajulikane madiwani wanalipwa nini? Kipengele hiki inaonekana Chemba wamelipwa hivi. Kongwa wamelipwa hiki, sisi tumelipwa hiki ndiyo maana watu wanavunjika moyo.

Amehoji ni kwa nini malipo yasijulikane kwa nchi nzima na kiwango kinacholipwa.

“Kama Kongwa Sh100,000 Chemba 100,000 tu, Tamisemi kutoa mwongozo kuliko kuacha mwenye uwezo alipe anavyotaka asiye na uwezo kujikaanga naomba mliangalie hili,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz